Wanajeshi wa Ukraine wateka Sloviansk

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Ukraine Petro Poroshenko

Rais wa Ukraine Petro Poroshenko ameelezea utekaji wa mji wa Sloviansk mashariki mwa Ukraine kutoka kwa wapiganaji wanaounga mkono Urusi kama mafanikio makubwa.

Amesema kuwa utekaji wa mji huo baada ya miezi mitatu ni hatua kubwa katika vita dhidi ya wanamgambo ambao wametishia ardhi ya taifa hilo.

Wapiganaji hao kwa sasa wamepiga kambi katika mji wa Donetsk kufuatia kutekwa kwa Sloviansk na mji wa Kromatosk ambao ulikuwa ngome kuu ya wapiganaji hao.

Wanasema kuwa walisalimu amri kwa lengo fulani lakini sasa wamekusanyika tena ili kupigana.