Athari za ukuwaji Afrika kwa wastaafu

Image caption Inawachukuwa muda mrefu wafanyakazi waliostaafu kulipwa malipo yao

Mkutano wa kimataifa wa maswala ya malipo ya uzeeni barani Afrika umeanza Jumatatu mjini Abuja nchini Nigeria. Hii ni mara ya kwanza mkutano kama huo kufanyika Afrika.

Kwa sasa Nigeria ndiyo nchi iliyo na uchumi mkubwa Afrika na ina nafasi kubwa ya kukuwa.

Lakini ukuwaji Afrika una athari kwa malipo ya uzeeni na masuala yanayoambatana na malipo hayo.

Dhamira ya mkutano huu ni mataifa kubadilishana ujuzi kati ya wataalamu wa malipo hayo kutoka Afrika na kushinikiza maendeleo katika masoko ya malipo ya uzeeni.

Image caption Nigeria ndiyo nchi iliyo na uchumi mkubwa Afrika

Ni nchi 30 zinazotoa malipo ya uzeeni kwa wafanyakazi wanaostaafu, wengi wao wakiwa katika umri mdgo uliotajwa kustaafu miaka 55.

Malipo miongoni mwa nchi

Mkutano huo unafanyika ikiwa nchini Uganda miongoni mwa mataifa mengine Afrika, wafanyakazi waliostaafu inawachukua mda mrefu kuanza kulipwa malipo yao, na wengine wana fariki kabla ya kupata malipo yao.

Kwa upande mwingine Afrika kusini inafahamika kuwa nchi inayotoa malipo makubwa ya uzeeni katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara.

Na kwa hivyo huenda Afrika ina uwezo wa kubadilishana mipango kutoka kwa nchi nyengine zilizo na uchumi wa kukuwa.

Sehemu ya kwanza ya mkutano huu uliopewa jina 'Africa Special', utaangazia mafunzo makuu yanayotokana miongoni mwa mataifa Africa, uwekezaji, jinsi ya kukabiliana na hatari, sheria muhimu, teknolojia na mawasiliano.

Mkutano huu utafanyika Afrika kwa miaka mitano ijayo kutoka kikao hiki cha kwanza cha ufunguzi.