Bangi halali katika jimbo la Washington

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bhangi ni halali katika majimbo 23 ya Marekani

Matumizi ya Bangi kwa ajili ya kujiburudisha yamehalalishwa katika jimbo la Washington nchini Marekani.

Washington ni jimbo la pili nchini Marekani kuhalalisha Bangi , baada ya Colorado, ambako jimbo hilo linajipatia mamilioni ya dola kila mwezi kwa kutoza ushuru biashara za Bangi kwa wanaoitumia kujiburudisha.

Hata hivyo utaratibu wa kuuza bidhaa hiyo utadhibitiwa ipasavyo katika jimbo hilo.

Ni maduka 25 pekee yaliyoruhusiwa kuuza Bangi hadi sasa, ingawa maafisa wanaamini kuwa idadi ya maduka huenda ikaongezaka na kufika miamoja.

Katika sehemu zingine za Marekani, majimbo 23 yanaruhusu matumizi ya Bangi kwa sababu za kimatibabu.