Kiongozi wa upinzani Ethiopia aonyeshwa kwenye TV

Image caption Andargachew Tsege alikamatwa akiwa safariki kutoka Milki za kiarabu

Kiongozi wa upinzani nchini Ethiopia, Andargachew Tsege, ameonekana kwenye televisheni ya taifa nchini humo kwa mara ya kwanza tangu Yemen kumkabidi kwa serikali mwezi jana.

Mkewe ambaye anaishi nchini Uingereza, Yemi Hailemariam, ameambia BBC kuwa ameshtuka kumuona mumewe kwa televisheni nchini humo.

Yemen ilimkamata Andargachew katika uwanja wa ndege wa Sanaa na kumkabidhi kwa Ethiopia.

Mnamo mwaka 2009,Andargachew alihukumiwa kifo kwa madai ya kupanga kuwaua maafisa wa serikali.

Andargachew, ambaye ni raia wa Uingereza na katibu mkuu vuguvugu haramu la Ginbot 7, alikanusha madai hayo.

Shirika la Amnesty International, wiki jana lilionya kuwa mwanasiasa huyo anakabiliwa na tiso la kuteswa ikiwa atazuiliwa nchini Ethiopia.

Bi Yemi alisema kuwa anahisi vibaya sana kuona picha ya mumewe.

"niliizima televisheini haraka sana, sikuweza kumuangalia, '' alisema Bi Yemi.

Bi Yemi, alisema uingereza ni sharti iagize kuachishwa mara moja kwa mumewe.

Andargachew alikuwa njiani kutoka Milki za kiarabu alipokamatwa katika uwanja wa ndege wa Sanaa mnamo tarehe 24 Juni.

Vuguvugu la Ginbot 7 lilizinduliwa tarehe 15 Mei baada ya uchaguzi wa mwaka 2005 ambao ulikumbwa na vurugu kufuatia madai ya wizi wa kura ambayo yalisababisha vifo vya watu 200.