Israel-Hamas wazidisha mashambulio

Haki miliki ya picha na
Image caption Wapalestina wakifyatua makombora zaidi katika miji ya Israel baada ya eneo lao la Gaza kushambuliwa

Wanamgambo wa Kipalestina wamefyatua makombora zaidi katika miji ya Israeli baada ya Israel kufanya mashambulio kadha ya anga katika maeneo ya Gaza mapema Jumatano.

Israel imesema imeyatungua makombora matano zaidi katika miji ya Tel Aviv na Ashkelon.

Maafisa wa afya katika eneo la Gaza wamesema mtu mmoja ameuawa katika shambulio la anga lilifanywa na majeshi ya Israel.

Wizara ya afya huko Gaza imesema Wapalestina wapatao 25 wameuawa na 70 kujeruhiwa katika uhasama wa hivi karibun kati ya Israel na Wapalestina.

Wizara hiyo ya afya imesema wanawake wanne na watoto watatu ni miongoni mwa watu waliouawa.

Tawi la kijeshi la Hamas limeonya kuwa Waisrael wote kwa sasa watalengwa na mashambulio yao.

Jeshi la Israel limesema kuwa usiku walibaini maroketi 118 yaliyokuwa yamefichwa, vituo kumi vya kijeshi vya Hamas na mahandaki 10.