Washukiwa wa kashfa ya tiketi matatani Brazil

Haki miliki ya picha AFP

Polisi nchini Brazil wanasema kuwa watu 12 akiwemo mkurugenzi wa kampuni iliyopewa mkataba wa kuuza tiketi hizo, wamesimamishwa kazi.

Hii ni kutokana na kashfa ya kuuza kiharamu tiketi za kutizama mechi za kombe la Dunia.

Ray Whelan, anayefanyia kazi kampuni hiyo inayoshirikiana na shirikisho la kandanda duniani FIFA, ametiwa mbaroni, na watu hao wengine katika mji mkuu Rio de Janeiro.

Sasa viongozi wa mashitaka wataamua iwapo watu hao watafunguliwa mashitaka au la.

Wakati huo huo, furaha imetanda kote Argentina baada ya timu hiyo kuiadhibu Uholanzi jumla ya mabao manne kwa mawili katika mechi ya nusu fainali usiku wa kuamkia leo.

Sasa Argentina itakabiliana na Ujerumani kutoka Uropa hapo siku ya Jumapili katika fainali ya kombe la Dunia mjini Rio.