Kerry kuokoa hali mambo Afghanstan

Haki miliki ya picha AFP GETTY
Image caption John Kerry

Waziri wa mashauri ya Nchi za kigeni wa Marekani, John Kerry, amefika Nchini Afghanistan ili kujaribu kutanzua hali ya taharuki inayokumba matokeo ya uchaguzi wa Urais unaokumbwa na utata.

Hali hiyo inaelezwa ilikuwa ikihatarisha hali ya amani ya taifa hilo.

Anatarajia kukutana na wagombea wawili wa Urais amabo kila mmoja ametangaza kushinda uchaguzi mkuu kufuatia shughuli za upigaji kura zilizomalizika mwezi uliopita.

Wagombea hao wawili ni Abdullah Abdullah na Ashraf Ghani.