HRW:'Watoto wa mitaani huteswa Uganda'

Watoto wanao randa randa mitaani nchini Uganda, hudhulumiwa na polisi pamoja na maafisa wengine wakuu.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch.

Polisi huwachapa kwa viboko na nyaya na kuwatupa gerezani na hata kuchukua hongo kutoka kwao.

Watoto hao wote, wasichana kwa wavulana hubakwa na wanaume watu wazima pamoja na vijana.

Afisaa mmoja nchini humo Mondo Kyateka, amesema kuwa watoto hao ni wahalifu sugu lakini polisi hawawezi kutumia nguvu kupitia kisi dhidi yao.

HRW limesema kuwa serikali inapaswa kuangazia njia za kuinua maisha ya watoto hao pamoja na kuwachukulia hatua wale wanaokiuka haki za watoto hao.

Zaidi ya nusu ya watu nchini Uganda wako chini ya umri wa miaka 15 na watoto watoto ndio wlio wengi wanaoishi katika hali ya umasikini.

Haijulikani idadi kamili ya watoto wanaoranda randa mitaani wako nchini Uganda, lakini utafiti unaonyesha mwaka 2013 idadi yao ilikuwa 10,000