GAZA:Israel yaendeleza mashambulizi yake

Haki miliki ya picha AFP GETTY
Image caption Wakimbizi wa Gaza

Maafisa wa Umoja wa mataifa katika eneo la Gaza wanasema kuwa idadi ya raia wa Palestina walioachwa bila makao na ambao kwa sasa wanatafuta makao kufuatia mashambulizi ya nchi kavu yanayotekelezwa na Israel sasa imeongezeka maradufu kutoka elfu ishirini na mbili hadi elfu arobaini.

Raia wengi wameelekea Magharibi mwa Gaza ili kutoroka mashambulizi ya Israel.

Baada ya utulivu siku ya ijumaa kuna ripoti kwamba mizingi ya israel imefanya mashambulizi mengine usiku kucha.

Zaidi ya raia 60 wa Palestina wakiwemo watoto tisa wanadaiwa kuuawa tangu kuanzishwa kwa oparesheni ya nchi kavu na hivyobasi kuongeza idadi ya watu waliouawa kufikia 300.

Jeshi la Israel linasema kuwa mwanajeshi mmoja wa Israel aliuawa siku ya ijumaa kufuatia ufyatulianaji wa risasi wa wenyewe kwa wenyewe.