Obama:Wanamgambo ndio walioangusha ndege

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais Barrack Obama

Rais Barrack Obama amesema kuwa ushahidi unaonyesha kwamba ndege ya Malaysia Airline iliokuwa ikisafiri kutoka Amstaderm kuelekea Kuala Lumpur ilitunguliwa na kombora lililorushwa kutoka eneo linalodhibitiwa na waasi wanaounga mkono Urusi.

Rais Obama amesema kuwa kitendo hicho kinatia hasira na kwamba waasi hao wamekuwa wakipokea usaidizi kutoka kwa Urusi ikiwemo makombora ya kuangusha ndege.

Obama ametaka usitishwaji wa vita nchini Ukraine ili kutoa fursa ya shirika huru la kimataifa kuchunguza kilichojiri.