Urusi yasema yapigwa vita vya maneno

Wafanyakazi wa UKraine wakiondoa miili ya abiria wa ndege ya Malaysia iliyoanguka Haki miliki ya picha AFP

Urusi imeshutumu mataifa ya Magharibi kuwa yanapigana vita vya maneno dhidi ya Urusi.

Wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema kuwa badala ya kuwalaumu wapiganaji wanaotaka kujitenga na wanaosaidiwa na Urusi, serikali ya Ukraine inafaa ieleze zana zake za kulenga ndege zilikuwa zinafanya nini katika eneo hilo?

Na katika tukio jengine, wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Urusi imetangaza kuwa inaweka vikwazo vya usafiri dhidi ya raia kadha wa Marekani, kulipiza vikwazo vya karibuni kabisa vilivowekwa na Marekani kwa sababu ya msukosuko wa Ukraine.