Afghanistan:Ukaguzi wa kura waahirishwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption John kerry[k] Abdulla Abdulla[c] Ashraf Ghani [r]

Tume ya Uchaguzi nchini Afghanistan imeahirisha kwa mda ukaguzi wa makaratasi ya kupiga kura katika uchaguzi wa Urais wa mwezi jana kutokana na kile kilichotajwa kama kutoelewana.

Mpango huo wa ukaguzi ambao ulianza siku nne zilizopita umekabiliwa na kujiondoa kwa wawakilishi wa pande pinzani katika shughuli hiyo.

Hatua hiyo ilichukuliwa kufuatia makubaliano wakati wa ziara ya waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry.

Mjumbe wa marekani James Dobbins amerudi nchini Afghanistan ili kujaribu kupeleke shughuli hiyo mbele.

Duru za kimataifa zinasema kuwa huenda ikachukua miezi kadhaa kabla ya mshindi wa Uchaguzi huo kutangazwa rasmi.