Hasara pande zote mbili katika Gaza

Gaza Haki miliki ya picha AP

Inaarifiwa kuwa Wapalestina kama 600 wameuwawa katika mtaa mmoja wa Gaza katika shambulio kubwa kabisa la mizinga tangu Israil kuanza mashambulio yake.

Makubaliano ya kusitisha mapigano baina ya Israil na Hamas huko Shejaiya ili kuruhusu magari ya wagonjwa kuingia huko, yalidumu saa moja tu, na yameanza tena.

Mwandishi wa BBC alioko Shejaiya anasema kabla ya mapigano kusita kwa muda mfupi, mizinga ya Israil ikifyatuliwa mfululizo na hivo kufanya jamii yote kukimbia.

Anasema nyumba nyingi sasa zimebaki kifusi tu.

Wakuu wa Palestina wanasema watu zaidi ya 400 wameuwawa Gaza katika siku 13.

Jeshi la Israil linasema askari wake 13 wameuliwa na wapiganaji Wapalestina katika Gaza.

Waziri Mkuu wa Israil, Benjamin Netanyahu amesema mashambulio ya Gaza yataendelea kwa muda unaohitajika.

Ripoti kutoka Qatar zinaonesha kutafanywa mkutano huko Jumapili baina ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, na rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, katika juhudi za kutafuta makubaliano ya kudumu ya kusitisha mapigano huko Gaza.

Qatar imekuwa kama mjumbe wa Hamas.

Kiongozi wa Hamas ambaye yuko uhamishoni, Khaled Meshaal, anaishi katika nchi hiyo ya Ghuba.

Wakuu wa huko wanasema wamepokea orodha kutoka Hamas ya shuruti zake kabla ya mapigano kusitishwa.