Watu wengine 4 wauawa Mombasa

Haki miliki ya picha d
Image caption Moja kati ya matukio ya mauaji yaliyowahi kutokea Mombasa

Watu wenye bunduki waliokuwa kwenye pikipiki wamewaua takriban watu wanne katika mji ulioko pwani ya Kenya Mombasa.

Polisi inasema watu hao walikuwa wakifyatua ovyo risasi kwa wapita njia.

Mji huo wa Bandari umeshuhudia ghasia katika miezi ya hivi karibuni huku kukiwepo mashambulio ya mabomu na ufyetuaji wa risasi ambayo wanamgambo wa alshabaab kutoka Somalia wanatuhumiwa kuyatekeleza.