Watu 25 wauawa kwa Bomu Nigeria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption wanamgambo wa kiislamu, Boko Haram

Takriban watu 25 wameuawa kwa shambulio la bomu mjini Kaduna nchini Nigeria, Polisi nchini humo wameeleza.

Bomu hilo lilimlenga Kiongozi wa dini ya kiislamu mwenye msimamo wa wastani Dahiru Bauchi ambaye alikua akitoka kuhubiri katika viwanja vya Murtala Muhammed

Bauchi amenusurika katika shambulio hilo, hajajeruhiwa halikadhalika haijajulikana waliotekeleza shambulio.

Wanamgambo wa kiislamu, Boko Haram wamekuwa wakitekeleza mashambulizi ya mabomu na mauaji nchini Nigeria tangu walipoanza Operesheni zao mwaka 2009 wakiwa na nia ya kuunda nchi ya kiislamu.

Boko Haram huwashambulia viongozi wa kiislamu ambao hukosoa misimamo yao.