Anti-Balaka,Seleka kusitisha mapigano?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wawakilishi kutoka kundi la Anti-Balaka na Seleka

Makundi hasimu ya wanamgambo na waasi nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati yamesaini makubaliano yenye lengo la kumaliza mzozo wa kidini baina yao uliodumu kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Makubaliano hayo yamefikiwa nchini Congo-Brazzaville kati ya waasi wa Seleka na wanamgambo wa anti-Balaka.

Mwandishi wa BBC amesema kuwa ingawa kumekua na makubaliano hayo bado mapigano yameendelea mjini Bambari.

Karibu robo ya watu milioni 4.6 wameyakimbia makazi yao.Pande zote mbili zimeshutumiwa kwa vitendo vya uhalifu wa kivita.

Makubaliano ya kuacha mapigano hayakudumu mjini Bambari, wanajeshi wawili wa zamani wa Seleka walishambuliwa kwa risasi na mmoja kuuawa, tukio hilo linadaiwa kutekelezwa na wapiganaji wa anti-Balaka.