Urusi yawekewa vikwazo

Haki miliki ya picha Getty

Canada imetangaza vikwazo dhidi ya Urusi kwa kile kinachodaiwa kupinga mashambulizi dhidi ya Ukraine.

Hatua hiyo imetangazwa na Waziri mkuu wa Canada Stephen Harper ambaye amesema vikwazo hivyo ni katika maeneo ya kiuchumi,nishati na makampuni ya silaha.

Harper amesema magaidi wanaendesha mashambulizi dhidi ya majeshi ya Ukrain.

Maofisa wa Jumuiya ya Ulaya wanatarajiwa kukutana leo ijumaa kujadili vikwazo Zaidi vya kimataifa dhidi ya Urusi.