Boko H:Wanachama 14 wafungwa Cameroon

Haki miliki ya picha
Image caption Kiongozi wa Boko Haram Sheikh Abubakar Shekau

Serikali ya Cameroon imewapeleka jela wanachama 14 wa kundi la Boko Haram na kuwapa kifungo cha kati ya miaka 10 hadi 20.

Washtakiwa hao walihukumiwa na jopo la kijeshi katika mji wa kazkazini wa Maroua,karibu na mpaka wa Nigeria kwa mashtaka ya kumiliki silaha na kupanga njama za kutekeleza uasi.

Idadi kubwa ya washukiwa wa kundi la Boko Haram imekamatwa kazkazini mwa Cameroon katika majuma ya hivi karibuni kufuatia mashambulizi katika vituo vya polisi na mauaji.

Siku ya jumatano ,Nigeria,Niger,Chad na Cameroon zilikubaliana kubuni jeshi la umoja ili kukabiliana na tishio kubwa linalosababishwa na Boko Haram.