Mke wa mwanasiasa atekwa Cameroon

Wanajeshi wa Cameroon Haki miliki ya picha AFP

Jeshi la Cameroon linasema kuwa kundi la wapiganaji Waislamu la Nigeria, Boko Haram, limemteka nyara mke wa mwanasiasa mashuhuri kaskazini mwa nchi.

Mke wa naibu waziri mkuu, Amadou Ali, na msaidizi wake wa nyumbani, walitekwa katika mji wa Kolofata, karibu na mpaka wa Nigeria.

Inaarifiwa kuwa mapigano baina ya Boko Haram na wanajeshi wa Cameroon yanaendelea.

Boko Haram imefanya mashambulio kadha kaskazini mwa Cameroon; na Jumamosi wafuasi zaidi ya 20 wa Boko Haram walifungwa nchini Cameroon baada ya kukutikana na hatia ya kupanga mashambulio.