Freetown:Mgonjwa wa Ebola afariki

Haki miliki ya picha None
Image caption Mwathiriwa wa Ebola Saudato Koroma kushoto

Maafisa wa afya nchini Sierra leone wamethibitisha kwamba mgonjwa mmoja wa Ebola aliyetoroka hospitalini katika mji mkuu wa Freetown amefariki baada ya kurudi hospitalini.

Mwanamke huyo kwa jina Saudato Koroma ndio mtu wa kwanza kupatikana na ugonjwa huo mjini humo.

Alijiwasilisha hospitalini humo baada ya serikali kuwataka raia kupitia tangazo la redio kusaidia kumsaka.

Alifariki Wakati alipokuwa akisafirishwa na wazazi wake mashariki mwa Sierra Leone ambapo vituo vya kuwauguza wagonjwa wa Ebola vimejengwa.

Ugonjwa huo umewaua zaidi watu 660 Magharbi mwa Afrika mwaka huu.