Israel kusitisha vita kwa saa 24 zaidi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waziri mkuu nchini Israel Benjamin Netanyahu

Serikali ya Israel imekubali kusitisha vita katika eneo la Gaza kwa sababu za kibinaadamu lakini kundi la Hamas limesema kuwa halitakubali tena makubaliano mengine.

Afisa mwandamizi nchini Israel amesema kuwa makubaliano hayo ya kusitisha vita yatafanyika kwa saa 24 kufuatia ombi la Umoja wa mataifa.

Siku ya jumamosi Hamas iliheshimu makubaliano ya kusitisha vita ya saa 12 lakini ikaendeleza mashambulizi yake ya makombora ya roketi nchini Israel mda huo ulipokamilika.

Msemaji wa Hamas ameiambia BBC kwamba uharibifu unao-onekana katika eneo la Gaza wakati wa mchana ndio uliowashinikiza kuendelea na mashambulizi hayo.

Ameishtumu Israel kwa kutumia makubaliano hayo kutekeleza mashambulizi zaidi.

Takriban raia 1000 wa Palestina wameuawa huku zaidi ya raia 40 wa israel wengi wao wakiwa wanajeshi wakifariki.