Wapiganaji wa Hamas waendeleza mapigano

Haki miliki ya picha AFP

Makundi ya wapiganaji wa Hamas yameendeleza mashambulizi zaidi huku pande zote mbili zikishutumiana kuvunja makubaliano ya kusitisha vita hivyo.Kuna taarifa kwamba vikosi vya Gaza na Palestina vilikuWa vikirusha makombora Israel.

Lakini kuna dalili kwamba mapigano hayo yametulia pamoja na madai kuwa pande zote mbili hazijakubaliana kusitisha kuhusiana na tofauti zao ili kusitisha mapigano.

Akizungumza na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa njia ya simu na Rais wa Marekani Barak Obama amesema hatua za haraka za kusitisha mapigano hayo na misaada ya kibinaadamu ni muhimu kwa sasa,kuliko wakati mwingine wowote.