Gazeti lataka Marekani kuhalalisha bangi

Image caption Raia wa Marekani

Gazeti moja maarufu nchini Marekani ,new York Times limetaka bangi kuhalalishwa nchini humo.

Katika taarifa yake ya kitengo cha uhariri, gazeti hilo limehusisha marufuku ya dawa hiyo na ile ya utumizi wa pombe katika miaka ya 20 na 30, likidai kuwa hatua hiyo imeleta madhara makubwa kwa jamii.

Linasema kuwa Bangi haina madhara hatari ikilinganishwa na pombe na tumbaku na kwamba kukamatwa kwa wanaomiliki dawa hiyo kunawaathiri pakubwa vijana weusi .

Majimbo ya Colorado na Washington tayari yameruhusu uuzaji wa bangi kwa lengo la kujiburudisha.