Kombora lalipua matenk ya mafuta,Libya

Haki miliki ya picha AFP

Vikosi vya zima moto vya Libya vinapambana kujaribu kuuzima moto baada ya kombora la roketi kulipua tanki la kuhifadhia mafuta wakati wa mapigano kati ya makundi mawili yanayohasimiana katika mji mkuu Tripoli.

Tanki hilo ni miongoni mwa matanki yanayomilikiwa na Kampuni ya mafuta ya serikali ya Libya yenye lita milioni sita za mafuta. Msemaji wa Kampuni hiyo Mohamed Al-Hariri amesema iwapo moto huo utasambaa kwenye matanki mengine ya karibu huenda ukasababisha madhara makubwa katika eneo lenye upana wa kilomita tano.

Serikali ya muda ya Libya imetaka ustishaji wa mapigano katika eneo hilo la maafa ili kuruhusu vikosi vya zima moto kufanya kazi yao bila kuingiliwa.