Israel:Tutajilinda na Hamas

Haki miliki ya picha AP

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Israel inatakiwa kujiandaa kwa ajili ya mpango wa muda mrefu katika Gaza.

Hata hivyo ameelezea msimamo wake dhidi ya kundi la wapiganaji wa Hamas. Netanyahu amesema Hamas wanapaswa kusambaratishwa na hilo ndilo lengo la Israel.

‘Tulijua kuwa tungekuwa na siku ngumu, hii ni siku ngumu na ya maumivu kutokana na mashambulizi haya, nguvu na malengo vinatakiwa ili kuendeleza mapambano dhidi ya kundi hilo, anasisitiza Netanyahu. Wizara ya afya ya Gaza imesema kuwa raia 10 wa palestina wameuawa katika shambulio la makombora yaliyolenga uwanja wa mpira yakitekelezwa na Israel..

Kati ya waliouawa katika shambulio hilo ni watoto saba waliokuwa wakicheza uwanjani hapo ambapo walipigwa na kufa papo hapo.

Hamas imeilaumu Israel kwa shambulio hilo,huku msemaji wa Israel akidai kuwa shambulio hilo lilitekelezwa kwa bahati mbaya.