Marekani yaishutumu Urusi

Haki miliki ya picha Getty

Marekani imeishutumu Urusi kuwa ilivunja makubaliano ya mwaka 1987 kwa kufanya majaribio ya makombora ya nyukilia ya umbali wa kati ya kilomita 500 hadi 5,500.

Tamko hilo la Marekani limekuja wakati nchi za Ulaya zikikubaliana kuiwekea vikwazo zaidi Urusi kutokana na mzozo wa Ukraine.

Msimamo huo unadai kuwa hauoni kama Rais Putin ana mpango wa kubadili sera zake. Maelezo zaidi yatakamilishwa katika mkutano wa mabalozi wa umoja wa ulaya lakini inafikiriwa kuwa huenda vikwazo vipya vikalenga sekta ya ulinzi, nishati na benki. Taarifa zinasema nchi nyingi za umoja wa Ulaya wameongeza mkazo zaidi katika vikwazo dhidi ya urusi baada ya kuangushwa ndege ya Malaysia huko Ukraine.