Jamhuri ya Dominica yateketeza silaha

Haki miliki ya picha AP

Jamhuri ya watu wa Dominica imeteketeza silaha za moto zaidi ya laki mbili ikiwa ni hatua ya kukabiliana nautamaduni wa uzaagaji wa silaha za moto.

Bunduki zilizoteketezwa katika kampeni hiyo ni za kutoka maeneo mbalimbali nchini ambazo zilisagwa na vyuma vyake vinatarajiwa kujengwa kumbukumbu katika mji wa Santo Domingo.

Waziri wa sharia nchini humo Francisco Dominguez ameuelezea utamaduni wa watu kumiliki silaha kuwa ni janga katika usalama wan chi hiyo.

Polisi wanasema asilimia 70 ya uhalifu unaofanyika nchini humo kila mwaka hutekelezwa kwa kutumia silaha hizo. Nchi hiyo inakadiriwa kuwa na silaha laki mbili kati ya raia milioni 10.