Sierra Leone yatangaza hali ya tahadhari

Haki miliki ya picha Science Photo Library
Image caption Rais wa Sierra Leone ametangaza hali ya tahadhari

Rais wa Sierra Leone ametangaza hali ya tahadhari kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Rais Ernest Bai Koroma ametoa agizo maeneo yaliyokuwa yakwanza kuripoti ugonjwa huo yadhibitiwe ipasavyo na kutengwa .

Rais Koroma aliagiza watu wasiruhusiwe kuingia au kutoka kwenye maeneo hayo chimbuko la mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Maafisa wa Usalama ndio waliopewa jukumu la kutekeleza maagizo hayo kwa ushirikiano na maafisa wa Afya ya umma.

Kulingana na takwimu Ebola huua asilimia 90% ya watu walioambukizwa homa hiyo ambayo huchukua kuanzia siku 2-20 kujulikana iwapo mtu ameambukizwa.

Image caption Rais wa Sierra Leone ametangaza hali ya tahadhari

Hadi kufikia sasa Ugonjwa huo umewaua zaidi ya watu 672 katika matifa matatu ya Afrika Magharibi yaani Liberia Sierra Leone na Guinea huku mtu mmoja akifariki nchini Nigeria.

Rais Koroma ametangaza kuwa hataenda Marekani kwa mkutano baina ya viongozi wa Afrika na rais Obama.