Shambulizi sokoni Gaza laua watu 15

Image caption Shambulizi Gaza laua watu 15 katika soko

Takriban watu 15 wameuwa na wengine 160 kujeruhiwa vibaya katika shambulizi kali la angani lililotekelezwa na Israeli kwenye soko moja huko Gaza .

Kwa mjibu wa viongozi wa Kipalestina mlipuko mkubwa ulilipua soko moja la Shejaiya la kuuza matunda na mboga ambalo kwa kawaida huwa na idadi kubwa ya watu, mashariki mwa Gaza.

Msemaji wa wizara ya afya Nchini Palestina amesema kuwa idadi kubwa ya wapalestina waliouwawa ama kujeruhiwa walikuwa wakiendesha shughuli za ununuzi wa bidhaa.

Msemaji wa kundi la Hamas, linalothibiti maeneo hayo Sami Abu Zuhri amekatalia mbali muafaka wa amani na kutaja kuwa hauna maana.

Wanahabari wanasema kuwa haijafahamika bayana iwapo wapalestina walikuwa wakijua kuwa watashambuliwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Shambulizi Gaza laua watu 15

Walioshuhudia wanasema kuwa, waliona moshi mkubwa ukifuka kutoka eneo hilo huku magari ya kutoa huduma ya kwanza yakionekana yakiingia na kutoka mahalipa tukio.

Aidha inasemekana kuwa mmoja wa waandishi habari ameuwawa katika shambulio hilo.

Wakati huo huo, majeshi wa nchi kavu ya Israel yamesema yatasitisha mapigano kwa muda wa masaa manne, lakini kauli hiyo haitotumika katika maeneo ambako wanajeshi wake wanaendeleza operesheni.