Eid: 24 wakanyagwa hadi kufa Guinea

Haki miliki ya picha
Image caption Watu 24 wakanyagwa hadi kufa mjini Conakry Guinea

Takriban watu 24 wamekufa mjini Conakry Guinea baada ya umati kukanyagana katika sherehe ya kuadhimisha kukamilika kwa mfungo wa ramadhan.

Image caption 24 waaga katika sherehe ya Eid

Watu wengine wengi walijeruhiwa ufukweni kandokando ya kitongoji cha Ratoma ambapo maelfu ya watu walikusanyika kusherehekea.

Shamra shamra hizo zilihudhuriwa na kundi la wanamziki la Instinct Killers ambao walikuwa kivutia kwa uma.

Utawala nchini humo umefunga fuo zote mjini Cananky na kumfuta kazi kiongozi wa shirika lililoandaa sherehe hizo.

Kumetangazwa pia wiki moja ya maombolezi.