Tumeharibu Mahandaki ya Hamas:Israel

Haki miliki ya picha Reuters

Msemaji wa Majeshi ya Israel Luteni Kanali Peter Lerner amesema wameharibu karibu nusu ya mahandaki 30 yanatumiwa na Hamas kuvuka mpaka.

Askari 10 wa Israel wameuawa wakiwamo pia watano kutoka kundi la Hamas walikouwa wamevuka kwa kutumia mahandaki hayo na kuingia Israel. Jeshi la Israel linaaminimaandaki hayo yanaunganisha mtandao huo. Luteni Kanali Peter amesema wanafanya kila namna kulizuia hilo.

Amesema Hamas wamekuwa wakijenga Mahandaki hayo kwa zaidi ya miaka miaka miwili na kwamba wanatakiwa kuyasambaratisha. Ametoa uthibitisho kuwa nusu ya maandaki 30 waliyoyagundua tayari wamekwisha kuyaharibu.