UN: Shule yake yashambuliwa Palestina

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uharibufu ulionywa Gaza na majeshi ya Israel

Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa kutoka eneo la Gaza wameiambia BBC kuwa wana Shule ya Umoja wa Mataifa ambayo maelfu ya wapalestina walikuwa wameifanya kama makazi imepigwa na makombora ya Israel.

Maafisa wa afya katika utawala wa Palestina wanasema kuwa takriban watu 15 wameuawa na wengine zaidi ya sabini kujeruhiwa.

Bob Turner anasema mtawanyiko wa silaha ambazo zimekuwa zikipigwa zinaashiria zimepigwa kutoka maeneo majeshi ya Israel yalipo.

Amefafanua kuwa shambulia hilo ni tukio lisilo la haki.

Zaidi ya watu lfu tatu walikuwa wamechukua hifadhi katika shule hiyo iliyoshambuliwa bila kutolewa kwa onyo lolote.

Jeshi la Israel liinasema askari wake walikuwa wakijibu mapigo baada ya wapiganaji wa kipalestina wakiwashambulia kutoka katika shule. Hata hivyo amesema tukio linaendelea kuchunguzwa.

Zaidi ya wapalestina elfu moa 200 wameuawa huku sehemu kubwa ya ukanda wa Gaza ikiharibiwa.