Misri yaandaa mkutano wa Gaza

Wapalestina waangalia mabaki ya jengo liloshambuliwa Jumamosi na Israil, kusini mwa Gaza, huko Rafah Haki miliki ya picha AFP

Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi, amesema kuwa pendekezo la nchi yake la kusitisha mapigano ndio suluhu nzuri kabisa ya kumaliza umwagaji damu huko Gaza.

Rais Sisi aliwaambia waandishi wa habari kwamba hakuna suluhu nyengine mbali ya mpango wa Misri.

Msemaji wa Hamas alieleza kuwa ujumbe wa Wapalestina utawasaili Cairo hii leo.

Waakilishi wa Marekani, Qatar na Uturuki piya wanatarajiwa kushiriki katika mazungumzo hayo ingawa haijulikani ikiwa Israil itatuma ujumbe Jumamosi.

Wakuu wa matibabu wa Gaza wanasema Wapalestina zaidi ya 200 wameuwawa katika mashambulio ya makomboya ya Israil tangu Ijumaa, baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kuvunjika.

Hapo awali jeshi la Israil lilisema kinga ya makombora ilizuwia makombora mawili yasifike Tel Aviv na moja lisipige Beersheba.