Marekani kusaidia Israel kujilinda

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Iron Dome

Marekani imepitisha mswada unaotoa msaada wa kifedha kwa Israel kuimarisha mfumo wake wa kujilinda dhidi ya makombora.

Mswada huo unatoa dola millioni mia mbili na ishirini na tano kuimarisha mfumo huo ambao umetumiwa kuyatungua makombora kadhaa ya roketi kutoka kwa wapiganaji wa kipalestina katika majuma ya hivi karibuni.

Mpango huo wa fedha hatahivyo ni sharti upitishwe na bunge la wawakilishi na kutiwa sahihi na rais Obama.

Waandishi wanasema kuwa wabunge wa Marekani wamekuwa wakiunga mkono Israel hivyobasi mswada huo huenda usikabiliwe na vikwazo vyovyote.