Mkuu wa mafuta Nigeria afukuzwa kazi

Kinu cha mafuta cha Nigeria Haki miliki ya picha Getty

Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria amemfukuza kazi mkuu wa shirika la mafuta la taifa, Andrew Yakubu, pamoja na manaibu wake watatu.

Serikali haikutoa taarifa rasmi kuhusu maafisa hao kutolewa kazini katika shirika hilo la Nigerian National Petroleum Corporation, NNPC, lakini kunafuatia tuhuma nyingi za ulaji rushwa.

Wananchi wa Nigeria walilalamika mwezi Februari pale gavana wa benki kuu wakati huo aliposema kuwa dola bilioni 20 zimetoweka katika NNPC.

Wakuu wa NNPC walikanusha hayo, lakini waandishi wa habari wanasema maelezo yaliyotolewa na wakuu hao hayakuaminiwa na wadadisi.