Mlipuko wa bomu Mogadishu wawauwa 3

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mlipuko mjini Mogadishu

Bomu moja lililokuwa limefichwa katika mfuko wa plastiki limelipuka katika mji mkuu wa Somali ,Mogadishu na kuwauwa takriban wanawake watatu waliokuwa wakilisafisha jiji hilo huku wengine 11 wakijeruhiwa.

Mfuko huo ulikuwa umechanganywa na takataka karibu na soko moja ambapo wafanyikazi wa kulisafisha jiji hilo hukutana.

Haijulikani ni nani aliyeegesha bomu hilo,lakini kundi la Alshabaab limetekelza mashambulizi kadha katika mji wa Mogadishu katika kipindi cha hivi karibuni.