Huwezi kusikiliza tena

Kunyonyesha kunaokoa maisha ya watoto

Dunia inaadhimisha wiki ya umuhimu wa kunyonyesha kwa lengo la kuwahamasisha akina mama kunyonyesha watoto wao pamoja na kuhakikisha afya ya watoto inaimarishwa kote duniani.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa takriban watoto 800,000, walio chini ya mwaka mmoja wanaweza kuokolewa kila mwaka kwa kunyonyeshwa.

Shirika la Unicef linakadiria kuwa asilimia 36,ya watoto Kusini mwa jangwa na Sahara wanafaidika sana kwa kunyonyeshwa ikilinganishwa na asilimia 38 ya watoto kote duniani.