Israel kusitisha vita kwa saa saba

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Eneo la Gaza lilivyoharibiwa na mashabulizi ya Israel

Israel imetangaza kile ilichokiita kusitisha vita kutokana na sababu za kibinadamu katika maeneo mengi ya Gaza kwa saa saba, kuanzia siku ya jumatatu asubuhi.

Afisa ngazi ya juu wa Kijeshi amesema makubaliano ya kusitisha mapigano hatahusu maeneo ya ya Kusini mwa Gaza katika mji wa Rafah na kwamba Israel inaweza kujibu mapigo kama itashambuliwa.

Awali pande zote Umoja wa Mataifa na Marekani walilaani kitendo cha Israel kushambulia karibu na shule iliyokuwa chini ya Umoja wa Mataifa katika eneo la Gaza, ambayo Wapalestina walisema kuwa watu kumi waliuawa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameita ukiukwaji wa maadili na kitendo cha jinai ambapo Marekani imesema ni kitendo cha kustusha.

Majeshi ya Israel yamesema yalikuwa yakilenga makundi matatu ya wapiganaji wa Islamic Jihadi walikuwa karibu na Shule hiyo.