Mradi hewa wa Mbuni wamtia mashakani Afrika:K

Image caption Martin aliwahadaa wakuu wa makampuni kumpa pesa kwa mradi hewa wa Mbuni

Mwanaume aliyekuwa mafichoni akishutumiwa kujihusisha na biashara chafu ya fedha na biashara za dawa za kulevya Martin Evans amekamatwa na Polisi nchini Afrika kusini baada ya kuwa mafichoni kwa miaka mitatu.

Evans, 52 kutoka Swansea nchini Uingereza, ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 21 mwaka 2006 kutokana na makosa ya uhalifu wa biashara ya dawa za kulevya na udanganyifu alikamatwa mjini Johannesburg Jumamosi.

Evans alidanganya wawekezaji 87 na kuwaibia Pauni 900,000, katika kile alichodai kuwa mradi wa Mbuni Kusini mwa Wales.

Mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani baadaye leo, viongozi wa mashitaka wakitaka arejeshwe kwao ambako kesi hiyo itaendelea kusikilizwa.

Evans alikua miongoni mwa watu wanaosakwa nchini Uingereza mwaka 2012 , Polisi ikihisi kuwa Evans amekua akiishi maisha ya anasa visiwa vya Cyprus.

Alitoweka mwezi Agosti mwaka 2011 baada ya kushindwa kurudi jela mjini Wiltshire baada ya kuruhusiwa wikendi.

Evans alikamatwa Jumamosi usiku katika operesheani iliyofanywa na idara ya taifa ya kupambana na uhalifu ikishirikiana na idara ya ujasusi chini ya Polisi wa Afrika kusini.