Amnesty:Jeshi Nigeria limetenda uhalifu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jeshi la Nigeria limedaiwa kutenda uhalifu wa kivita

Shirika la Amnesty International linasema kuwa limepata ushahidi wa uhalifu wa kivita Kaskazini mashariki mwa Nigeria, ambapo wanajeshi wanakabiliana na kundi la wapiganaji wa kiislamu- Boko Haram.

Pande zote mbili zinalaumiwa kwa makosa hayo.

Katika video moja ya kuogofya, watu waliodaiwa kuwa wanajeshi wa Nigeria na wapiganaji wanaoungwa mkono na serikali, waliwachinja kinyama wafungwa waliokuwa wamewazuilia.

Serikali ya Nigeria inasema kuwa unyama huo hauna nafasi katika jeshi huku ikiahidi kufanya uchunguzi.

Boko Haram pia linalaumiwa kwa kufanya unyama mkubwa dhidi ya binadamu.

Amnesty inalaumu tume huru ya uchunguzi katika kile inachokiita misururu ya ukiukaji wa haki za kibinadamu kutoka kwa pande zote mbili.