UNHCR:Watu wengi wanatoroka Ukraine

Umoja wa mataifa umesema kuna ongezeko la idadi ya watu wanaokimbia mapigano Mashariki mwa Ukraine.

Shirika la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR linasema katika kipindi cha miezi miwili iliyopita pekee watu 100,000 waliamua kuyahama makazi yao kutokana na kukosekana kwa usalama katika miji ya Luhansk na jimbo la mikoa ya Donetsk.

Hata hivyo mapema mwezi june 2600 waliondoka katika makazi yao pia. Huduma za kibinadamu zinatia mashaka.

UNHCR inasema baadhi ya raia hao waliokimbia wanakosa huduma mhimu kama vile maji, magodoro na vifaa vingine vinavyoweza kuwalinda na magonjwa ya mlipuko.