Westgate:Stakabadhi za usajili zilibiwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Westgate:Stakabadhi za usajili wa simu za magaidi zilibiwa

Watu wanne wanaokabiliwa na mashtaka ya kuwasaidia wavamizi walioshambulia maduka ya Westgate walighushi stakabadhi za usajili walizotumia kusajili nambari za simu zilizotumika na wavamizi kuwasiliana na washirika wao.

Kusikizwa kwa kesi hiyo ilianza mwezi januari na hadi kufikia sasa mahakama imesikiza ushahidi kutoka kwa watu walioshuhudia tukio hilo ambalo lilitekelezwa na wapiganaji wa kundi la Al -Shabaab.

Watu 67 walifariki katika shambulizi hilo la septemba mwaka jana.

Hussein Hassan Mustafa, Mohammed Ahmed Abdi, Liban Abdullah Omar na Adan Mohammed Abdikadir — walikuwepo mahakamani wakijadiliana miongoni mwao katika lugha ya kisomali.

Image caption Mashahidi wanasema magaidi walitumia stakabadhi zao kusajili nambari za simu zilizotumika na magaidi.

Wanne hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama ya kutekeleza shambulizi la kigaidi ,kuwa wanachama wa kundi haramu na kuwa na vifaa vinavyotumika kutekeleza mashambulizi ya kigaidi.

Afisa mmoja wa polisi na mwanamke mwanamuziki walitoa ushahidi wa kuwa stakabadhi zao zilitumika kinyume na matarajio yao kusajili nambari za simu zilizotumika kupanga na kutekelezwa kwa shambulizi hilo.

"Kwa kweli sijui ilikuwaje ikawa walitumia stakabadhi zangu rasmi kusajili nambari hiyo ya simu," alisema mwanamziki huyo Rose Mukere.

Bi Mukere ni mwimbaji wa nyimbo za injili.

Kundi la Alshabab lilijigamba kuwasiliana na wapiganaji hao wanne walioteka jengo hilo la maduka katika eneo la Westlands jijini Nairobi.

Image caption Watu wakikimbilia maisha yao siku ya shambulizi la kigaidi.

Zaidi ya Mashaidi 35 wametoa ushahidi wao huku 15 zaidi wakitarajiwa kufika mbele ya mahakama hiyo.

Kundi la Alshabab linasema lilitekeleza mashambulizi hayo ikitaka kuishinikiza serikali ya Kenya kuondoa majeshi yake nchini somalia ambapo inahudumu chini ya nembo ya Umoja wa Afrika .

more expected to give evidence, prosecuting lawyers said.

Kesi itaendelea Agosti tarehe 20.