Nahitaji nyumba ya Qunu: Winnie

Image caption Winnie Mandela

Mjane wa Hayati Nelson Mandela Winnie Madikiela-Mandela anadai kumiliki nyumba iliyopo kijijini Qunu kwa madai kuwa ni kwaajili ya watoto wake.

Mwanasheria wa Winnie Madikiela amesema madai ya mteja wake yana haki zote kwa mjibu wa haki za kimila.

Eneo hilo la makazi ambalo mjane wa Mandela anadai linakadiriwa kuwa na thamani ya rand 46m sawa na dola milioni 4.3 ama paundi million 2.5.

Hayati Mandela aliachana na Winnie mwaka 1996 na kujaliwa kuwa mabinti zao wawili ambao ni Zinzi and Zenani.

Katika wosia wake enzi za uhai wake Hayati Mandela alisema

Eneo lake la Qunu litatumika na familia yake daima ili kuimarisha umoja wa familia na Mandela.

Hata hivyo Mwansheria aliandika wosia huo Dikgang Moseneke hajazungumzia lolote kuhusiana na mvutano huo.