Asprini inapunguza vifo kutokana na Saratani

Watafiti nchini Uingereza wanaofanya utafiti kuhusu matumizi ya dawa ya Asprin kupunguza magonjwa, wanapendekeza kuwa watu walio na umri wa zaidi ya miaka 50 wanapaswa kushauriana na daktari kuhusu matumizi yake kila siku ya maisha yao.

Wanaamini kwamba dawa hiyo inaweza kupunguza idadi ya watu wanaopata Saratani hasa Tumboni.

Watafiti hao kutoka Chuo kikuu cha Queen Mary jijini London, wanachunguza data zote zinazopatikana kielimu na majaribio kadhaa ya kliniki iwapo dawa ya Aspirin ina uwezo wa kutibu baadhi ya maradhi.

Wanasema kuwa ni jambo la busara kuweza kukomesha baadhi ya vifo vinavyotokana na maradhi ya mshtuko wa Moyo au kuvuja damu Tumboni.