Samsung na Apple kufutiana kesi US

Kampuni ya Apple na Samsung zimeafikiana kutupilia mbali kesi zote zilizofunguliwa Marekani zikiwa zimeshitakiana.

Kampuni hizo zilizozana kuhusu uanzilishi wa vifaa vya kielektroniki katika nchi kadhaa ikiwemo Uingereza, Korea ya kusini, Japan na Ujerimani.

Kampuni zote mbili zilikuwa zimewasilisha mashitaka mahakamani lakini katika taarifa yao ya maafikiano ya hivi punde, kampuni zote mbili zimesema mzozo huo haukua na jambo lolote linalohusiana na leseni na hivyo basi zitaondoa kesi hizo Marekani.

Mwafaka huu kati ya kampuni hizo mbili umeafikiwa baada ya miaka kadhaa ya migogoro.

'Migogoro kadhaa'

Migogoro yao ilianza mwaka 2011 baada ya Apple kuishtaki Samsung huko Marekani na kudai kuwa kampuni ya Galaxy iliyoko Kusini mwa Korea ilitumia miundo ya iPhone na iPad.

Kampuni ya Galaxy ilijibu mashtaka ya Apple na kuishtaki kwa misingi ya kuingilia haki zake za uanzilishi wa programu za picha, muziki, na picha za video, na pia jinsi ya kunasa na kutuma picha za video mtandaoni.

Apple pia iliwasilisha mashtaka ya kupinga madai ya uanzilishi na Galaxy lakini hatimaye kuafikiana kutupilia mbali kesi hizo za uanzilishi.

'Kuangazia Marekani'

Hata hivyo, mgogoro kati ya kampuni hizo mbili ulio mkubwa zaidi unaendelea katika mahakama za Marekani.

Apple ilishinda kesi mbili dhidi ya Samsung miaka michache iliyopita.

Mwezi Mei, mahakama moja ya Marekani iliamuru Samsung kulipa dola million 119.6 kwa Apple kwa kuingilia haki zake za uanzilishi. Apple ilikuwa imewasilisha ombi kulipwa dola milioni 2.2.

Vile vile, mahakama hiyo ilikataa kauli kuwa Apple iliingilia haki Fulani za Uanzilishi wa Samsung na kulipa Samsung dola 158,000.

Hata hivyo Samsung ilikana mashtaka hayo na kutaka kulipwa dola milioni 6 kwa madai kuwa Apple ilingilia haki zake za Uanzilishi wa simu Fulani za kisasa zinazoweza kunasa na kupeperusha picha za video

Miaka miwili iliyopita, baraza lingine la waamuzi liliamuru Samsung kulipa Apple dola bilioni 1.05 kwa kutumia maarifa ya Apple kutengeneza vifaa vyao, kinyume na sheria.

Baraza hilo la uamuzi lilikata kauli kuwa vifaa vya kielekroniki vya Samsung vilitumia programu ya iPhone-maker ambayo ni ya Apple na kupuuza madai ya Samsung dhidi ya Apple kuwa program hiyo ni yao.

Uamuzi huo bado unapingwa na Samsung.