Zambia yapata kocha mpya

Timu ya taifa ya Zambia imepata Kocha mpya, Honour Janza aliyechukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Patrice Beaumelle aliyeondoka mwanzoni mwa juma hili.

Rais wa Shirikisho la soka la Zambia Kalusha Bwalya amesema ni changamoto kubwa waliyonayo lakini wana imani na Janza.

Janza anakutana na kibarua cha kwanza katika michuano ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika ya mwaka 2015.

Zambia iko kundi F na itaikaribisha Msumbiji tarehe 6 mwezi Septemba, kisha itaelekea Cape Verde siku nne baada ya mechi hio.

Chipolopolo imefikia hatua ya kumtafuta mrithi wa Beaumelle baada ya mfaransa huyo kuamua kuungana na aliyekua kocha wa zambia Herve Renard ambaye kajiunga na Ivory Coast.

Bwalya amesema hana hofu kuwa Janza ambaye alikua Mkurugenzi wa ufundi ndani ya shirikisho la soka la zambia atamudu kuipeleka Zambia mbele.