Ebola yatikisa mfumo wa afya Liberia

Haki miliki ya picha European Photopress Agency
Image caption Watalaam wa afya katika tahadhari ya ugonjwa wa Ebola

Waziri wa Habari wa Liberia Lewis Brown ameiambia BBC kwamba mfumo wa afya wa nchi hiyo umeyumbishwa na athari zilizotokana na mlipuko huo wa ugonjwa wa Ebola.

Kikosi cha jeshi nchini humo kimetawanywa kuweza kuwazuia watu wasisafiri kuingia katika mji mkuu wa nchi hiyo, kutoka katika maeneo ya vijiji yaliyokumbwa na ugonjwa huo.

Wakati huohuo katika nchi jirani ya Sierra Leone, ambayo maeneo yote yamewekwa vizuizi kujaribu kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo. Waziri wa Habari wa nchi hiyo Alpha Kanu amesema inakatisha tamaa kuona kwamba dawa ambazo bado ziko katika majaribio, hazijasambwazwa nchini himo.