Afueni kwa wajakazi Brazil

Image caption Wajakazi Brazil wapata afueni

Sheria mpya ambapo waajiri watatozwa faini iwapo watashindwa kuwasajili wafanyikazi wao wa nyumbani imeanza kutekelezwa nchini Brazil.

Ni miongoni mwa hatua mpya zinazolenga kuwalinda wafanyakazi hao wapatao milioni sita.

Waajiri sasa wanaweza kupigwa faini ya mamia ya madola kila mara wanapokiuka sheria hiyo.

Mwaka uliopita marekebisho ya kikatiba yaliwapa wafanyakazi wa nyumbani takriban masaa 44 ya kufanya kazi kwa wiki.

Sheria hiyo mpya imesababisha familia nyingi kuwaajiri wafanyikazi zaidi ili kufanya kazi kwa zamu huku waajiri wakilazimika kufanya kazi za ziada.

Mwaka jana mageuzi ya kikatiba yaliwawezesha wafanyakazi wa nyumbani kufanya kazi kwa masaa 44 kwa wiki.

Pia walipata haki nyinginezo kama kufanya kazi kwa saa nane kwa siku , kupata kiwango kizuri cha mshahara , kupumzika wakati wa mchana, kulipiwa malipo ya uzeeni na faida nyingiezo.

Sehemu kubwa ya mabadiliko haya imetekelezwa lakini bado kuna changamoto.

Ikiwa mfanyakazi atafutwa kazi bila sababu , basi mwajiri wake atalazimika kulipa asilimia 40 zaidi ya mshahara wake pamoja na asilimia nyingine kumi kwa serikali.

Sheria hizi bila shaka zimefanya hali kuwa ngumu kwa wajiri na hivyo baadhi yao wanajifanyika kazi zao.