Watu sita wauawa katika ghasia Somali

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wapiganaji wa Al-shabaab

Takriban watu sita wameuawa katika ghasia katikati mwa Somali.

Ijumaa usiku, wanamgambo kutoka kundi la Alshabaab walishambulia kambi moja ya wanajeshi wa Umoja wa Afrika katika mji wa Buloburde ,yapata kilomita 200 kazkazini mwa mji mkuu wa Mogadishu.

Vikosi vya Amisom viliuteka mji wa Buloburde kutoka kwa Alshabaab mapema mwaka huu,lakini wanamgambo hao bado wanadhibiti eneo kubwa la viungani mwa mji huo.

Wameendelea kutekeleza mashambulizi mjini Mogadishu ili kujaribu kuiondoa serikali inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa.