Mchekeshaji nguli Robin Williams afariki

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Robin Williams enzi za uhai wake akiwa ameshikilia tuzo ya Oscar.

Salamu za rambi rambi zimeendelea kumiminika kufuatia kifo cha nguli wa uigizaji na vichekesho nchini Marekani Robin Williams, ambaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka sitini na sita.

Polisi wanaamini kwamba Robin amejiua yeye mwenyewe akiwa nyumbani kwake katika mji wa Carlifonia.

Gwiji wa utengenezaji filamu Steven Spielberg amefafanua kwamba Williams alikua na kipaji cha namna ya kipekee katika sanaa ya uchekeshaji na alikua ni muigizaji maarufu sana .

Naye Rais wa Marekani Barack Obama alimuelezea Williams kwamba katika uchekeshaji wake alikua akigusa maisha ya watu.

Robin Williams katika uhai wake alikua maarufu sana na mcheshi katika kipindi cha runinga kilichojulikana kama 'Mork and Mindy' kabla hajageukia katika tasnia ya filamu kama ya Good Morning Vietnam na pia alikua ni mshairi na mashairi yake yalikua ya kuvunja mbavu.

Mchekeshaji huyu katika siku ama miaka ya mwisho ya uhai wake alikua katika mapambano ya utumizi wa dawa za kulevya na hivi karibuni alikua akisumbuliwa na msongo wa mawazo.